What's up guys, hope you're fine.
Leo ni siku nyingine tena, ambayo nitaendelea kushare njia tofauti tofauti za kutengeneza pesa mtandaoni
Nipende kuendelea kusisitiza kwamba mtandaoni kuna pesa nyingi mno, ila watu wengi hasa kutoka nchi za dunia ya tatu hawajaweza Kutambua Namna ya kuzipata huko mtandaoni.
Soma pia: Bila kufahamu hizi mbinu huwezi kutengeneza pesa mtandaoni.
Kwa uzoefu wangu kuhusu masuala ya Kutengeneza pesa mtandaoni nimegundua vijana wengi hawana skills au ujuzi wa kuweza kuchimba (extract) hizo pesa mtandaoni.
Ngoja nisiwachoshe Sasa tuangalie kile nilichotaka kuwaelezeni leo.
Jinsi ya kutengeneza pesa mtandaoni kupitia app ya Airbnb
Umeshawahi kusikia kuhusu app ya Airbnb? ni imani yangu kuwa watu wachache wanaifahamu app hii na ni asilimia chache wanaojua Namna ya kutengeneza pesa mtandaoni kupitia app hii.
Airbnb ni nini?
Kwa ambao ni mara ya kwanza kusikia kuhusu app hii, ni kwamba ni app inayowasaidia wageni au watalii kupata sehemu ya kulala au kupumzika kupitia kukodi chumba au vyumba kupitia mtandaoni.
Kutokana na kukua kwa sekta ya utalii duniani na pia kuongezeka kwa idadi ya watu wanaosafiri duniani, imefanya bei za hotel au sehemu za makazi gharama kuongezeka.
Hivyo basi kwa mfano kama mtalii hajawahi kufika Tanzania, anapofika kwa mara ya kwanza bila shaka kama hajui huduma za Airbnb atapelekwa kwenye hotel au lodge au ambayo anatozwa hela kubwa.
Kwa kutambua tatizo hilo Airbnb kwa sasa inawarahisishia watalii ku order vyumba au chumba kwa bei nafuu zaidi kuliko ile ambayo mtalii angetozwa anapoingia kwenye hotel kubwa.
Soma pia: Njia 7 halali za kutengeneza pesa mtandaoni.
Siyo kwamba app hii inamsaidia mtalii kupata chumba cha kulala bali pia inaweza kukusaidia wewe msomaji wa makala hii kutengeneza pesa mtandaoni kupitia app ya Airbnb.
Swali la kujiuliza Je nitatengenezaje pesa kupitia app ya Airbnb?
Jibu ni rahisi kama una vyumba vyako ambayo havitumiki na vina ubora wa kuridhisha unaweza kuviorodhesha ndani ya app ya Airbnb na kujiongezea kipato pale mtalii atakapohitaji kwenda sehemu ambayo vyumba vyako vipo akiridhishwa na chumba au vyumba vyako anakutafuta atalipia na wewe kupata pesa kupitia app hii.
Still confused,
App hii inafanyaje kazi,
Iko hivi unapojisajili kwenye app hii unajaza taarifa za huduma ya malazi au makazi unazotoa.
Kwa mfano,
√ Aina ya nyumba unayoitaka kuikodisha kwa wageni je ni Apartment au bungalow
√Je hiyo nyumba ina vyumba vingapi?
√Je hali ya hivyo vyumba ikoje ni self contained room ama,
√Mahali au sehemu vilipo vyumba vyako vya kukodisha wageni mfano Mtaa, wilaya,Mkoa na nchi sehemu yako ya makazi inapopatikana.
Biashara hii ya kukodisha nyumba au vyumba sio ngeni kwa Tanzania na haijawa maarufu sana. Lakini inafanyika hasa zile sehemu zenye vivutio vya utalii na sehemu ambazo huwa mmiminiko wa wageni Mfano Arusha, Zanzibar, Kilimanjaro, Morogoro, Dar es Salaam, Mwanza n.k
Soma pia: Njia za kutengeneza pesa kupitia blog 2020
Huwezi amini kupitia app hii watu wanaweza kutengeneza zaidi ya $300 kwa mwezi hii itatokana ubora wa vyumba vyako na ukarimu unaonesha kwa wageni ambao wamewahi ku order vyumba vyako.
Je nitawezaje kufanya Biashara hii wakati sina vyumba au lodge ambayo ina vyumba vya kulala wageni?
Hakika hilo ndo swali watu wengi wanajiuliza. It's simple.
Nina rafiki yangu anafanya hii business huu ni mwaka wa tatu sasa yeye alikuwa tour guider pale Arusha. Anasema wakati yeye anaanzisha biashara hii hakuwa na chumba, lodge yoyote. Swali la kujiuliza e alifanikiwaje ilihali hana vyumba?
Anasema mara ya kwanza alikuwa anatuma barua za maombi kwa wamiliki wa hotel, lodge na vyumba vya kulala wageni ili kama ikiwezekana wampatie vyumba kadhaa havitangaze ndani ya app ya Airbnb.
Baadhi ya wamiliki wa hotel lodge, waliomkubalia aliingia nao mkataba, alipokuwa analeta wageni au watalii kulala kwenye vyumba vya wamiliki wa zile hotel na Lodge alikuwa analipwa kiasi fulani.
Kutokana na pesa alizozikusanya ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu alijenga vyumba vyake mwenyewe kwa ajili ya kulala wageni na ameviorodhesha kwenye app ya Airbnb. Hivyo basi hana haja ya kutumia vyumba vya wamiliki wa hotel na Lodge.
Sound good?
Biashara hii ukiamua unaweza kuifanya na kujiongezea kipato mtandaoni.
Soma pia: Tumia njia hii kupata vocha ya 1000 kila siku mitandao yote.
Jinsi ya Kujiunga na AIRBNB
Unaweza kujiunga na fursa hii kwa kupitia link maalumu ambayo nimekuwekea Hapo chini.
Je nalipwaje?
Nadhani ndo swali ulilokuwa unajiuliza, je utapokeaje malipo yako?
It's simple,
Baada ya mteja kuweka order nyumba au vyumba vyako na akafanikiwa kufika hicho chumba au hiyo sehemu basi wewe utalipwa na pesa itakuwa inaonekana kwenye akaunti yako ya AIRBNB.
Jinsi ya kuitoa ni kwamba utachagua njia ya malipo ambayo inapatikana kwenye eneo lako. Ila mara nyingi wanalipa kupitia Pioneer au PayPal.
KUMBUKA: Kuna njia mbili za kutengeneza pesa kupitia app ya Airbnb
1. Malipo kwa wageni waliokodi chumba, vyumba au nyumba yako.
Soma pia: Faida na hasara za biashara ya mtandaoni.
Kama Ungependa kutengenezewa Youtube Channel au Blog/website usisite kuwasiliana nasi kwa email johonline2@gmail.com
HITIMISHO
Hivyo ndivyo app ya AIRBNB inayokuwezesha kutengeneza pesa mtandaoni. Hivyo basi kama umefurahia fursa hii ni mda wa kujipanga ili uweze kunufaika na fursa hii ya Kutengeneza pesa mtandaoni. Nachosisitiza hapa ni kwamba hakuna pesa itakayopatikana haraka bila kujituma, uvumilivu na kufanya kazi kwa bidii. Hivyo basi kama umejipanga kutengeneza pesa mtandaoni, hivyo ni vitu vya muhimu kuvizingatia.
Je una maoni au swali lolote? Tafadhali andika maoni au mchango wako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Tukutane kwenye makala hijayo panapo majaliwa. Au tuandikie kupitia email johonline2@gmail.com
2 Comments