Leo katika yetu tutazungumzia Namna ya kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog 2020.
Soma pia: Mambo matano ya kufahamu kabla hujalenga kutengeneza pesa mtandaoni.
Ni ukweli usiopingika kwamba mtandaoni kuna pesa nyingi sana, kinachotushinda walio wengi ni ujuzi au namna gani ya kuzipata hizo fedha.
Hivyo basi kwa Kutambua hilo nimekuandalia njia 5 halali za kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog 2020. Bila kupoteza muda tuanze kuzichambua njia hizo,
1. Kutengenezana kuuza Blog
Hii ni mojawapo ya njia ambayo unaweza kunitumia kutengeneza pesa mtandaoni ukiwa na blog. Kupitia njia hii utaweza kutengeneza blog na kwenda kuiuza kwenye masoko ya mtandaoni.
Kwa msaada wa haraka unaweza kuangalia video hii
Soma pia: Jinsi ya kupata Vocha ya 1000 Kila siku kwa kutumia smartphone
Ukiuza blog yako Flippa utakuwa umeweza kujiongezea kipato kupitia mtandaoni. Je ungependa kutengeneza na kuuza Blog yako mtandaoni? Ili ufanikiwe kirahisi
2. Kuomba Matangazo ya Google Adsence
Hii ni njia inayotumiwa na blogger wengi kutengeneza pesa mtandaoni. Hili kutengeneza pesa kupitia njia hii unatakiwa uwe na Blog, blog yako iwe na vigezo vinavyohitajika ili uwekewe matangazo kwenye blog yako.
Ukibahatika kupewa matangazo kwenye blog yako pale watu watakapotazama na kubonyeza matangazo kwenye blog yako utalipwa.Soma pia: Faida na hasara za biashara ya mtandaoni
Blogger wengi wanajua kwamba Google Adsence ni kampuni pekee ambayo unawekewa matangazo na kuanza kulipwa kiufupi zipo kampuni nyingine zinazofanya kazi kama Adsence mfano media.net, properaAds, Adsterra n.k
3. Kuuza mavazi yenye nembo yako.
Bloggers wakubwa wamekuwa wakitumia njia hii kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog.
Wanachokifanya ni kuchapisha tisheti na kuweka nembo zao. Baada ya hapo wanatangaza mavazi hayo kupitia blog zao, pindi watu wanaponunua mavazi hayo basi blogger hujipatia kipato. Miongoni mwa blogger wanaotengeneza pesa kwa njia hii ni Wode Maya kutoka Ghana.
4. Kuuza vitabu na kozi tofauti tofauti Mtandaoni
Miaka ya hivi karibuni biashara hii imepanuka kwa kwa kasi sana. Katika njia blogger uandika vitabu na kuandaa kozi tofauti tofauti na kuja kuzitangaza kwenye blog yake.
Soma pia: Jinsi ya Kutengeneza zaidi ya Shilingi 2000 kupitia app hii
Ili kupata hiyo kozi au kitabu anachouza lazima ulipie kiasi fulani cha pesa. Kutokana na hali hiyo blogger anakuwa amefanikiwa kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog.
5. Kuwa wakala wa Makampuni tofauti tofauti.
Pia ukiwa na blog unaweza kujisajili na kuwa wakala wa Makampuni ukawa unatangaza bidhaa zao kupitia blog yako. Ikitokea mteja akanunua bidhaa au huduma yoyote kupitia blog Yako unalipwa kiasi fulani cha pesa.
Kama unahitaji kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog na kuwa wakala hutojutia kujiunga na Clickbank, Jumia au Amazon.
Kama Ungependa kutengenezewa Youtube Channel au Blog/website usisite kuwasiliana nasi kwa email johonline2@gmail.com
HITIMISHO
Kitu cha msingi kufahamu kabla hujalenga kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog, ni kwamba hakuna pesa ya harakaharaka mtandaoni. Kutengeneza pesa mtandaoni kupitia blog itategemea na bidii yako kwenye kazi, kujijengea ratiba na uvumilivu. Ni imani yangu kwamba ukingatia hayo niliyonena hspo juu utaweza kutengeneza pesa mtandaoni bila shida.
Je una maoni au swali lolote? Tafadhali andika maoni au mchango wako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Tukutane kwenye makala hijayo panapo majaliwa.
0 Comments