Je ungependa kuanza kujiongezea kipato mtandaoni? Kama jibu lako ni ndiyo basi makala hii inakufaa wewe. Hivyo basi fuatilia kwa makini. Baada ya kusoma makala hii, utaweza kutengeneza pesa mtandaoni bila wasiwasi, kwa sababu tumekuandalia mambo matano unayotakiwa kuyafahamu kabla hujalenga au kupanga kutengeneza pesa mtandaoni na njia tofauti tofauti za kutengeneza pesa mtandaoni.
Bila kupoteza muda, tuanze kuchambua mambo matano unayotakiwa kuyafahamu kabla hujalenga kutengeneza pesa mtandaoni;
1. Suala la mtaji.
Njia nyingi za kutengeneza pesa mtandaoni mara nyingi hazihitaji mtaji mkubwa.
Unaweza kuanza biashara ya mtandaoni ukiwa na smartphone yako, au kompyuta na kifurushi cha intanenti.
Mfano wa njia za kutengeneza pesa mtandaoni bila kuwa na mtaji wa ela kubwa ni pamoja na kufungua Youtube Channel, kupakua application zinazouliza maswali na wewe kulipwa baada ya kujibu maswali pamoja na kuwa mkufunzi, ili kufundisha watu Namna mbalimbali za kutengeneza pesa mtandaoni.
Jifunze jinsi ya Kutengeneza youtube channel hapa
Pia kuna njia nyingine za kutengeneza pesa mtandaoni unatakiwa uwe na mtaji wa kutosha kabla hujapanga kutumia njia hiyo kutengeneza pesa mtandaoni. Kwa mfano kuanzisha duka la mtandaoni kama vile KIKUU au Alibaba, unatakiwa uwe umejipanga kiuchumi.
2. Usiwe na Tamaa ya kupata pesa haraka
Watu wengi hushindwa kufanikiwa kutengeneza pesa mtandaoni, kwa sababu wamejawa tamaa ya kutengeneza pesa haraka haraka. Hii hutokea pale anapoona mwenzake amefanikiwa kupitia kutengeneza pesa mtandaoni, na yeye uamua kufanya vile vile bila kujua kwamba huyo aliyemuiga alipitia vikwazo gani hadi hakafanikiwa.
Hivyo basi unatakiwa upunguze tamaa uwe mvumilivu huku ukiendelea kufanya kazi kwa bidii, huku ukikumbuka wahenga walisema "mvumilivu hula mbivu".
3. Fanya utafiti au uchunguzi
Kabla ya kuamua kutengeneza pesa mtandaoni,suala la kufanya utafiti haliepukiki. Kwa mfano kama umeamua kutengeneza pesa mtandaoni kupitia kufungua Youtube Channel, blog au website unatakiwa kufanya utafiti kidogo kuhusu vitu ambavyo watu wengi kwenye jamii yako wanafatilia Sana.
Kwa mfano kama watu kwenye jamii yako wanapenda kufatilia masuala ya michezo, burudani, afya au afya unaweza kuamua kutengeneza youtube channel, website au blog ukielezea masuala hayo. Kama unapanga kuanzisha duka la mtandaoni hakikisha unafanya utafiti kuona ni bidhaa gani jamii ya inahitaji sana.
4. Usikate Tamaa
Kama umejipanga na umeamua kutoka moyoni mwako kutengeneza pesa mtandaoni, basi hutakiwi kukata tamaa, ukikata tammaa ndoto zako za kujiongezea kipato kupitia kutengeneza mtandaoni zitayeyuka kama barafu.
Hali hii ndio imefanya vijana wengi kushindwa kutengeneza pesa mtandaoni.
Kwa mfano unakuta kijana ametengeneneza youtube channel au blog anapost mara tatu au tano anaanza kukata tamaa ghafla. Hili utengeneze pesa mtandaoni epuka kukata tamaa.
5. Jenga mtandao ( Network)
Kuwa na mtandao wa watu ili kutangaza biashara zako mtandaoni, inategemea na njia gani unaitumia kutengeneza pesa mtandaoni.
Kama unafanya biashara ya kuuza sarafu za kigeni maarufu kama Forex huna haja ya kuwa na mtandao mkubwa wa watu. Lakini kama unalenga kutengeneza pesa mtandaoni kwa kupitia kutengeneza youtube channel au blog ndugu yangu unatakiwa kuwa na mtandao mkubwa wa watu watakao kuwa wanafatilia channel yako, website au blog ili ikuongezee nafasi kutengeneza pesa mtandaoni.
Kama Ungependa kutengenezewa Youtube Channel au Blog/website usisite kuwasiliana nasi kwa email johonline2@gmail.com
Hitimisho
Ni imani yangu kama umefanikiwa kusoma makala hii mwanzo hadi mwisho, utakuwa umepata maarifa ambayo yatakusaidia katika safari yako ya kuanza kutengeneza pesa mtandaoni. Utaweza kufanikiwa kutengeneza mtandaoni kama utazingatia yale yaliyoandikwa katika makala hii mfano, kutokukata tamaa, kufanya utafiti na kuzingatia ratiba yako uliyojitengea kwa kwa ajili ya kutengeneza pesa mtandaoni.
Je una maoni au swali lolote? Tafadhali andika maoni au mchango wako Hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Tukutane kwenye makala hijayo.
1 Comments