Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Jinsi ya Kutambua Mtu Aliyeshika Simu yako bila Yeye Kujua

 Je unahisi kuna mtu anashika simu yako kipindi haupo? leo katika makala hii utaelewa Namna ya kumtambua mtu ambaye ameshika simu yako bila yeye kujua kwamba umemtambua.

Soma pia: Vitu unavyotakiwa kuwa navyo ili kutengeneza pesa mtandaoni.


Who touched my phone


Njia hii inafanyaje kazi?

Baada ya kupakua app hii ambaye link yake nitaiweka chini, utajisajili kwenye app hii, utaruhusu app hii kupiga picha  baada ya hapo utaanza kufaidi kazi za app hii.

Angalia hii video kwa maelezo zaidi


         Soma pia: Jinsi ya Kuweka Password Kila Sehemu (kila app) Kwenye simu yako. .

Faida za App hii

App hii itafanya kazi zifuatazo;

√Kupiga picha mtu yeyote atakayegusa simu yako, hivyo ukiiwasha simu yako itakuonyesha picha ya mtu ambaye ameshika simu yako.

√Kama simu yako ina nywila (password) mtu yeyote akijaribu kuweka password ikakataa app hii itampiga picha na kuweza kuiona utakapofungua app hii.

√App hii itakuonyesha app au program zote ambazo mtu ambaye ameshika simu yako amezitumia kwa mfano kama amefungua app ya Message, WhatsApp, Instagram app hii itakuonyesha.

√Kumbuka app hii inafanya kazi kama simu yako ina password.

            Cha muhimu zaidi kuhusu app hii ni kwamba inampiga mtu picha bila ya yeye kuona kama amepigwa picha.

Soma pia: Tumia njia hizi kutengeneza pesa mtandaoni kila siku.

Je app hii inapatikana wapi?


Jinsi ya Kutambua Mtu Aliyeshika Simu yako bila Wewe Kujua

App hii utaipata kupitia google play store. Ingia Google Play store tafuta app inayoitwa "Who Touched My Phone" ipakue na kuinstall kwenye simu yako huweze kuwatambua watu wanaotumia simu bila wewe kujua.



HITIMISHO

Hadi kufikia hapo ni imani yangu utakuwa umeelewa jinsi ya kuongeza ulinzi kwenye simu yako kwa kuweza kuwatambua watu wanashika au kutumia simu yako bila ya wewe kujua.


Soma pia: Jinsi ya kupata Vocha ya 1000 kila siku.



Kama Ungependa kutengenezewa Youtube Channel au Blog/website usisite kuwasiliana nasi kwa email johonline2@gmail.com

Je una maoni au swali lolote? Tafadhali andika maoni au mchango wako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Tukutane kwenye makala hijayo panapo majaliwa.



Post a Comment

0 Comments